Shirika la Ndege la Kenya na la Emirates jana yametangaza kusaini mkataba wa ushirkiano ambao utaleta machaguo mengi zaidi kwa wateja wao kusafiri kati ya Afrika na Mashariki ya Kati, na kuwawezesha abiria wa mashirika yote mawili ya ndege kufikia maeneo mapya yanayounganishwa na huduma ya mashirika hayo kwa tiketi moja tu.
Chini ya mkataba huo, abiria wa Emirates sasa wataweza kusafiri kwenda sehemu 28 zikiwemo Nampula, Bangui, Bujumbura, Kigali n.k, chini ya huduma ya Shirika la Ndege la Kenya kwa kupitia Nairobi, huku abiria wa Shirika la Ndege la Kenya wakiweza kwenda sehemu 23 zikiwemo Singapore, Tokyo, Bangkok n.k. kupitia Dubai chini ya huduma ya Emirates.