Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Maendeleo ya Kiserikali (IGAD) Workneh Gebeyehu amesema, athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi zinafanya hali iliyopo ya uhaba wa chakula kuwa mbaya zaidi katika kanda ya Afrika Mashariki.
Gebeyehu amesema hayo kwenye hotuba aliyoitoa katika Mkutano wa 14 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa IGAD, uliofanyika nchini Djibouti jana Jumatatu. Aliwaambia viongozi waliohudhuria mkutano huo kwamba majanga mengi ya asili na hali ya kibinadamu katika kanda hiyo ni matokeo ya uharibifu wa mazingira, mabadiliko ya tabianchi, na hali mbaya ya hewa, hasa mzunguko wa ukame na mafuriko.
Alisema kabla ya kuzuka kwa mzozo nchini Ukraine na wa hivi karibuni huko nchini Sudan, dunia tayari ilikuwa na idadi kubwa ya wakimbizi wa hali ya hewa kuliko wakimbizi wa migogoro.