Watoto takriban milioni 14.2 nchini DRC wahitaji misaada ya kibindamu
2023-06-14 09:02:36| CRI

Shirika la hisani la kimataifa Save the Children jana lilitoa taarifa likisema kuwa watoto takriban milioni 14.2 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wanahitaji misaada ya kibinadamu.

Taarifa hiyo imesema wakati mgogoro umekuwa ukiendelea katika sehemu kadhaa nchini humo kwa karibu miongo mitatu, watoto ndio wanaodhurika zaidi. Kufuatia shambulizi lililofanywa mapema Jumatatu na waasi dhidi ya kambi moja ya wakimbizi mashariki mwa jimbo la Ituri, ambalo limesababisha mauaji ya raia wasiopungua 46 wakiwemo watoto 23, shirika hilo limetoa wito kwa wafadhili kutoa fedha za ziada mara moja ili kusaidia manusura kupata huduma ya afya, vifaa vya kupikia na kuunga mkono shughuli za kuunganisha familia kwa ajili ya watoto waliotengana na walezi wao.