Kenya yazindua mpango wa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana wanaotafuta ajira mtandaoni
2023-06-14 09:02:16| CRI

Kenya jana Jumanne ilizindua mpango wa wiki tano wa kutoa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana wanaotafuta ajira za mtandaoni kutoka nje ya nchi.

Waziri wa Leba na Huduma za Jamii Florence Bore amesema mpango huo umevutia vijana zaidi ya elfu mbili kwa lengo la kuwawezesha kwa ujuzi, ustadi na mitazamo inayohitajika kwenye kazi za mtandaoni kuwahudumia wateja wa nje ya nchi.

Waziri huyo ametoa mwito kwa vijana wa Kenya kukumbatia teknolojia ya habari ili kutafuta fursa za kiuchumi zinazopatikana kupitia majukwaa ya kidijitali.