Pande zinazopigana nchini Sudan zakataa pendekezo la IGAD la kutoa suluhu ya kisiasa kwenye mgogoro
2023-06-14 08:52:49| CRI

Pande mbili zinazopigana nchini Sudan zimepinga pendekezo la Mamlaka ya Maendeleo ya Kiserikali (IGAD) ambalo linatoa suluhu ya kisiasa kwa mapigano yanayoendelea.

Pendekezo hilo likiwa na mwongozo wa utatuzi wa mapigano ya Sudan limepitishwa katika kikao cha 14 cha kawaida cha Wakuu wa nchi na serikali wa IGAD kilichofanyika nchini Djibouti.

Mwongozo huo unajumuisha kuanzishwa kwa kamati ya pande nne inayoongozwa na Kenya ili kufuatilia nyaraka za Sudan, kupanga mikutano ya ana kwa ana kati ya pande mbili hasimu za Sudan, na kuanzisha mchakato jumuishi utakaotatua kwa njia ya kisiasa mgogoro wa Sudan ndani ya wiki tatu.

Hata hivyo, kwenye taarifa yake, wizara ya mambo ya nje ya Sudan imekataa Kenya kushika uongozi wa kamati ya pande nne, ambazo ni pamoja na Ethiopia, Djibouti na Sudan Kusini.

Kwa upande wa kikosi cha Msaada wa Haraka RSF, kimekataa pendekezo la jumuiya hiyo, kikitoa mwito wa kuunganisha pendekezo hilo na lingine lililotolewa na Marekani na Saudi Arabia.