Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) ya Tanzania, Khamis Hamza Khamis, amesema Zanzibar inatarajia kunufaika na Biashara ya Kaboni wakati wowote kuanza sasa.
Akizungumza katika ikao cha Bunge linaloendelea mjini Dodoma, Bw. Khamis amesema Msitu wa Jozani uliopo Unguja na Msitu wa Ngezi katika Kisiwa cha Pemba inaweza kutumika kuvuna hewa ya ukaa na kuwapatia faida wananchi wa visiwani humo.
Naibu Waziri huyo amebainisha kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar inatarajia kutoa elimu wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.