Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ), kimeandaa kongamano maalum kinapoungana na nchi nyingine barani Afrika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika kwa kusisitiza ulinzi wa mtoto katika nyanja zote.
Kongamano hilo linafanyika leo Juni 15, linawashirikisha watoto, asasi za kiraia, taasisi za kiserikali, wazazi, walimu na viongozi wa dini, ambapo kaulimbiu ya TAMWA Zanzibar katika maadhimisho hayo ni “Matumizi Sahihi ya Kidijitali kwa Ustawi Bora wa Mtoto.”
Takwimu zilizotolewa mwezi Januari na ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zinaonesha kuwa, kati ya matukio 1,360 ya ukatili yaliyoripotiwa mwaka jana, jumla ya watoto 1, 173 waliathirika na vitendo vya udhalilishaji na ukatili.