Hii ni ahadi iliyotolewa na rais Xi Jinping wa China mwezi Machi mwaka 2019 wakati alipokutana na Spika wa Baraza la chini la Bunge la Italia. Ahadi hiyo ina maana muhimu, na kuonesha nia ya rais Xi ya kuwahudumia wananchi wa China.
Kutoka katibu wa tawi la Chama cha Kikomunisti cha China kijijini hadi kiongozi wa taifa la China, rais Xi siku zote anajichukulia kama mhudumu wa wananchi. Anafuatilia maisha ya watu, kujaribu kukidhi matakwa yao, na kuwa na mapenzi makubwa kwao, na amefanya kila analoweza ili wananchi wa China wapate maisha bora.
“Nikiwa kiongozi wa taifa, wananchi wamenipa kazi hii, ni lazima niwaweke juu zaidi moyoni mwangu,” alisema.