Huawei kusaidia Ghana ili kuongeza utoaji wa nishati kwa ufanisi
2023-06-15 08:46:46| CRI

Kampuni kubwa ya teknolojia ya China Huawei inashirikiana na sekta ya nishati ya Ghana ili kuhakikisha uzalishaji wa umeme na utoaji wa huduma vinafanyika kwa ufanisi.

Ushirikiano huo unatoa suluhu za kisasa za mawasiliano kwa Bwawa la Umeme la Bui, mojawapo ya mabwawa makubwa ya kuzalisha umeme wa maji nchini Ghana na chanzo kikuu cha umeme, ili kusaidia kuongeza ufanisi wake wa kufanya kazi. 

Kwa mujibu wa makamu wa rais wa Idara ya Mawasiliano ya Kampuni ya Huawei, Xie Ye, miundombinu ya kiteknolojia ya bwawa hilo ni mtandao wa mkonge wa mawasiliano usiotumia waya, ambao unaunganisha matabaka tofauti ndani na nje.

Naye naibu mkurugenzi wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia masuala ya umme, Seth Mahu, alielezea ushirikiano huo kama jambo jipya. 

Mradi wa Bwawa la Bui uliojengwa na kampuni ya China ulikamilika mwaka 2013.