Waziri Mkuu wa Palestina atoa wito wa kuchukuliwa hatua za kimataifa mara moja kulinda ufumbuzi wa nchi mbili
2023-06-15 09:15:49| CRI

Waziri Mkuu wa Palestina Bw. Mohammed Ishtaye jana alitoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka za kimataifa kulinda ufumbuzi wa nchi mbili ili kuepuka "hujuma za Israel."

Alisema hayo katika mkutano wake na mjumbe maalumu wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia amani ya Mashariki ya Kati Bw. Sven Koopmans uliofanyika huko Ramallah.

Bw. Ishtaye alisema kuna haja ya kuchukua hatua mara moja ili kulinda ufumbuzi wa nchi mbili wakati Israel inashinikiza Mamlaka ya Palestina isambaratike na kuondoa uwezekano wa kuanzisha nchi huru ya Palestina.