Nigeria yaripoti visa 1,629 vya ugonjwa wa kipindupindu
2023-06-15 22:46:04| cri

Kituo cha Kudhibiti na Kukinga Magonjwa cha Nigeria (NCDC) kimetangaza kuwa, jumla ya visa 1,629 vya ugonjwa wa kipindupindu, pamoja na vifo 48, vimeripotiwa nchini humo hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka huu.

Mkurugenzi Mkuu wa kituo hicho Ifedayo Adetifa amesema, majimbo 13 yameathiriwa, na kwamba Shirika la Afya Duniani (WHO) limechukua hatua za kuimarisha kudhibiti na kukinga mlipuko wa ugonjwa huo nchini humo. Hatua hizo ni pamoja na kuwekeza katika miundombinu ya maji safi na usafi wa mazingira, kufanya usafi, kutoa chanjo na matibabu, na kufuatilia mlipuko wa ugonjwa huo. Pia ameongeza kuwa, kipindupindu kinaweza kuzuilika, na wadau wote wanapaswa kuchukua hatua muhimu ili kuzuia kuenea kwake.