Wanafunzi 20 wa shule za sekondari Tanzania kushiriki kwenye kambi ya lugha ya Kichina ya majira ya joto 2023
2023-06-15 09:18:10| CRI

Jumla ya wanafunzi 20 kutoka shule mbili za sekondari za Tanzania wanaojifunza lugha ya Kichina watashiriki kwenye kambi ya lugha ya kichina ya majira ya joto mwaka 2023, chini ya uungaji mkono wa Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang, China.

Wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari ya Baobab na Shule ya Sekondari ya Wasichana ya St. Christina walifunga safari jana Jumatano kuja China kushiriki kwenye kambi hiyo ya wiki mbili ambayo inatarajiwa kuwaleta mjini Beijing na Jinhua mkoani Zhejiang.

Akiongea kwenye hafla iliyofanyika kabla ya kuondoka kwa wanafunzi hao, mkurugenzi wa Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Zhang Xiaozhen amesema, anatumai kuwa wanafunzi hao watapata hisia tofauti na manufaa baada ya kuitembelea miji ya Beijing, Shanghai na Jinhua.