Serikali ya Tanzania imezishukuru serikali ya China na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO kwa kuendelea kuunga mkono maendeleo ya elimu ya juu ya ufundi barani Afrika.
Naibu mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaamu William-Andey Lazaro Anangisye akimwalikisha katibu mkuu wa wizara ya elimu, sayansi na teknolojia Carolyne Nombo, amesema kuwa China na UNESCO zimeunga mkono maendeleo ya elimu ya juu ya ufundi barani Afrika kupitia Mradi wa Mfuko wa UNESCO na China CFIT, ambao sasa uko katika kipindi cha tatu.
Katika ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa siku tatu wa kipindi cha tatu cha Mfuko wa UNESCO na China uliofanyika katika chuo kikuu cha Dar es Salaam, Anangisye amesema kuwa mradi huo unalenga kuimarisha uwezo wa taasisi za elimu ya juu katika kuendeleza ufundishaji unaozingatia mahitaji ya soko la nguvukazi na ujifunzaji unaolenga kujiongezea uwezo, na kuimarisha uhusiano kati ya vyuo vikuu na sekta mbalimbali.
Mradi huo uliotengewa bajeti ya jumla ya dola milioni 7.5 za kimarekani umetekelezwa kwa miaka minne nchini Cote d'Ivoire, Ethiopia, Gabon, Senegal, Tanzania na Uganda.