Mhudumu wa wananchi
2023-06-16 10:49:18| cri

“Ni lazima nifuatilie wasiwasi wa wananchi, na ni lazima nitimize matumaini ya wananchi”, asema Rais Xi Jinping wa China.

Kazi zote za rais Xi zinahusiana na wananchi.

Wakati alipofanya kazi katika wilaya ya Zhengding mkoani Hebei, rais Xi alitembelea wilaya yote kwa kutumia usafiri wa baiskeli, ili kuwasiliana na watu na kujua matarajio yao. Mkoani Fujian, aliwaongoza maafisa wengine kwenda sehemu za mbali na maskini zaidi, ili kujua hali ilivyo ya maisha ya watu. Mkoani Zhejiang, aliongoza kazi ya uokoaji wakati kimbunga kilipotokea.

Tangu kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China, rais Xi alifanya ziara za ukaguzi katika sehemu za mashina zaidi ya mara 100, na kutembelea vijiji na miji mbalimbali. Anajali sana mambo yote yanayofuatiliwa na watu. Mara kwa mara anafanya kazi mchana kutwa na usiku kucha, hata anakosa muda wa kula.

Kazi yangu ni kuwahudumia wananchi, na inachosha, lakini pia inanifurahisha, alisema rais Xi. Ameongeza kuwa kila afisa anapaswa kufanya kazi kwa bidii, ili kuwatimizia wananchi mambo mengi zaidi.