Katibu mkuu wa UM atoa wito wa kuharakisha hatua za tabianchi
2023-06-16 09:12:07| CRI

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana alitoa wito wa kuharakisha hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi akieleza wasiwasi wake kutokana na kukwama kwa ufuatiliaji na kurudi nyuma duniani katika juhudi za kufikia ajenda ya tabianchi.

Ameeleza kuwa kupunguza ongezeko la joto duniani lisizidi nyuzi joto 1.5 bado kunawezekana na kupendekeza makubaliano na ajenda husika za kuongeza juhudi za ziada katika suala la tabianchi, ambazo zinataka serikali za nchi mbalimbali, sekta ya mafuta ya visukuku na wadau husika kutimiza ahadi zao.

Bw. Guterres amesisitiza kuwa nchi zilizoendelea lazima zihimize benki za maendeleo za pande nyingi kusaidia nchi zinazoendelea kupata ufadhili binafsi kwa gharama nafuu ili kuongeza uwekezaji katika sekta ya nishati endelevu.