Emir wa Qatar afanya ziara nchini Iraq
2023-06-16 09:19:47| CRI

Waziri mkuu wa Iraq Bw. Mohammed Shia al-Sudani jana huko Baghdad alikutana na Emir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani ambaye yuko ziarani nchini humo, ambapo pande hizo mbili zilijadili hatua za kuimarisha uhusiano kati ya nchi zao na kufikia makubaliano ya kuanzisha ushirikiano katika sekta za ujenzi wa miundo mbinu na utoaji wa nishati.

Akiongea na wanahabari Bw. al-Sudani alisema pande hizo mbili zilijadili fursa ya uwekezaji ya Qatar katika ujenzi upya wa Iraq na Iraq inatarajia kujiunga na miradi ya maendeleo ya Iraq nchini Qatar.

Mapema siku hiyo Bw. al-Sudani na Emir Sheikh Tamim waliongoza mazungumzo ya wajumbe wa nchi hizo mbili na kushuhudia kusainiwa kwa makubaliano ya ushirikiano.