Waziri wa Fedha nchini Kenya, Njuguna Ndung’u amesema kiwango cha mfumuko wa bei nchini humo kwa sasa kimefikia asilimia nane.
Amesema mfumuko huo umeshuka kwa kiasi kikubwa kutoka asilimia 9.6 mwezi Oktoba mwaka jana kutokana na hatua zilizowekwa na serikali ya nchi hiyo.
Waziri Ndung’u amesema Benki Kuu ya Kenya (CBK) kupitia kamati ya sera ya fedha, imeendelea kusimamia sera ya fedha kama sehemu ya hatua zinazowekwa ili kupunguza mfumuko huo. Amesema Benki hiyo itaendelea kutekeleza mageuzi yaliyoainishwa katika jitihada za kupunguza mfumuko wa bei.