Hali ya kibinadamu nchini Sudan bado yaendelea kuzorota
2023-06-16 08:54:35| CRI

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Masuala ya Kibinadamu na Mratibu wa Misaada ya Dharura, Martin Griffiths alisema Alhamisi kuwa wakati mgogoro nchini Sudan ukiingia mwezi wa tatu, hali ya kibinadamu kote nchini inaendelea kuzorota, na kuonya kuwa hali ya Darfur inazidi kuwa mbaya na kugeuka maafa ya kibinadamu.

Alisema takriban watu milioni 1.7 sasa ni wakimbizi wa ndani, nusu milioni ya watu wanatafuta hifadhi nje ya Sudan, na mamia ya raia wameuawa huku maelfu wakijeruhiwa. Aidha amebainisha kuwa uporaji wa vifaa vya matibabu na vya misaada ya kibinadamu unaendelea kwa kiwango kikubwa. Wakulima nao hawawezi kufikia kwenye ardhi yao, jambo ambalo linaongeza hatari ya uhaba wa chakula. Vilevile kumekuwa na ongezeko la ripoti za unyanyasaji wa kijinsia.