Serikali ya Tanzania kuondoa ushuru kwenye magari ya gesi, umeme
2023-06-17 21:52:08| cri

Serikali ya Tanzania inakusudia kusamehe ushuru wa bidhaa unaotozwa kwa mujibu wa uwezo wa injini kwenye magari yanayotumia nishati ya umeme pekee na magari yanayotumia nishati ya gesi asilia pekee.

Waziri wa Fedha wa nchi hiyo, Mwigulu Nchemba ameyasema hayo jana katika hotuba yake ya makadirio ya bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024. Amesema lengo la hatua hiyo ni kuhamasisha matumizi ya nishati ya umeme na gesi asilia nchini humo, na hivyo kuokoa matumizi ya fedha za kigeni zinazotumika kuagiza nishati ya mafuta kutoka nje ya nchi.