Kutoka “ kiongozi wa umma” hadi “mtumishi wa wananchi”
2023-06-18 17:20:04| CRI

Rais Xi Jinping wa China aliwahi kuambiwa na baba yake Bw. Xi Zhongxun kuwa “ hata kama wewe ukikuwa afisa wa ngazi ya juu, usisahau kufanya bidii kuwahudumia na kuwazingatia watu kwa dhati, na kuwasiliana na watu kwa urafiki”. Maneno hayo ni matakwa ya baba kwa mwanawe, na pia ni urithi kati ya vizazi viwili vya wanachama wa Chama cha Kikomunisti cha China.

Bw. Xi Zhongxun, aliyewahi kujulishwa na Mwenyekiti Mao Zedong wa China kuwa “kiongozi kutoka kwa umma”, ni mwanamapinduzi kutoka tabaka la wafanyakazi aliyezaliwa kuwa mwana wa wakulima wakati taifa la China lilipokabiliwa na hatari kubwa. Bw. Xi Zhongxun ana hisia kubwa kwa watu wa China hasa kwa wakulima, ambayo imeleta ushawishi mkubwa kwa mwanawe Xi Jinping.

“Kuwahudumia wananchi ni heshima kubwa zaidi wa wazazi”, hii ni matumaini ya Bw. Xi Zhongxun kwa mwanawe Xi Jinping. Rais Xi Jinping amekumbuka vizuri maneno hayo ya baba yake na siku zote amekuwa akiwaweka wananchi moyoni na kutimiza lengo la “kuwahudumia wananchi kwa moyo wote” kwa hatua halisi. Rais Xi aliwahi kusema kuwa “ni watu wa China ndio wanaamua mambo ya taifa na sisi ni watumishi wa umma wanaosaidia wananchi wetu kushughulikia mambo mbalimbali”.

Kati ya vizazi viwili vya baba na mwana, kutoka “ kiongozi wa umma” hadi “mtumishi wa wananchi”, kilichorithiwa ni hisia na nia dhati za kuwahudumia wananchi.