Sudan yaongeza muda wa kufunga anga yake hadi Juni 30
2023-06-18 21:52:29| cri

Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya nchini Sudan imeongeza muda wa kufungwa kwa anga yake hadi mwisho wa mwezi huu, huku mapigano kati ya Jeshi la Sudan na Kikosi cha RSF yakiendelea.

Anga ya Sudan imefungwa tangu mapigano yalipotokea kati ya pande hizo mbili April 15, kufuatia mfumo wa uongozaji wa ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Khartoum kuathiriwa na mapigano hayo.

Kwa mujibu wa Muungano wa Madaktari nchini humo, watu 958 wameuawa na wengine 4,746 kujeruhiwa tangu mapigano yalipotokea kati ya Jeshi la Sudan na kikosi cha RSF katika mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum, na maeneo mengine nchini humo.