Idadi ya watu waliofariki kutokana na joto kali nchini India yakaribia 100
2023-06-19 09:37:43| CRI

Idadi ya watu waliofariki kutokana na joto kali katika mkoa wa Utter Pradesh na Bihar nchini India imeongezeka na kufikia 98 katika siku tatu zilizopita.

Maofisa kutoka mikoa hiyo miwili wamesema, watu 54 wamefariki katika mkoa wa Utter Pradesh, huku watu 44 wakifariki katika mkoa wa Bihar kutokana na joto kali.

Takwimu za Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini India (IMD) zimeonyesha kuwa, kiwango cha juu cha joto katika baadhi ya sehemu za nchi hiyo kilifikia nyuzi 42.2 Ijumaa na Jumamosi, ikiwa ni nyuzi 4.7 zaidi ya joto la kawaida.

Habari zinasema, karibu watu 400 walilazwa katika hospitali ya wilaya ya Ballia, mkoani Utter Pradesh katika siku tatu zilizopita, na walikuwa wanasumbuliwa na homa, kushindwa kupumua, na matatizo mengine ya kiafya yanayotokana na joto kali.