Kambi ya majira ya joto ya wanafunzi wa sekondari ya Taasisi ya Confucius UDSM yafunguliwa rasmi mkoani Zhejiang
2023-06-20 15:34:25| cri

Halfa ya ufunguzi wa kambi ya majira ya joto ya wanafunzi wa sekondari ya Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ilifanyika Julai 19 katika Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang, China. 

Wanafunzi na walimu 20 kutoka Tanzania wameshiriki kwenye kambi hiyo iliyoandaliwa na Kitivo cha Kimataifa cha Utamaduni na Maendeleo ya Jamii katika Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang. Akiongea kwenye ufunguzi wa kambi hiyo, Mkuu wa chuo hicho Prof. Wang Hui amewakaribisha wageni hao kutoka Tanzania, na kuitakia mafanikio shughuli hiyo. Naye mwalimu wa Tanzania anayeongoza msafara huo Bi. Goodness Leonard Mfanga amekishukuru Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang kwa maandalizi mazuri ya shughuli hiyo, na pia ameeleza matarajio yake kwa shughuli zijazo katika kambi hiyo.  

Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Utamaduni na Jamii Duniani ya Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang Profesa Wang Hui akitoa hotuba

 

Mwalimu wa Tanzania Goodness Leonard Mfanga akitoa hotuba 

Siku hiyo alasiri, wanafunzi kutoka Tanzania walitembelea maktaba, makumbusho ya historia ya Chuo Kikuu na Jumba la Makumbusho la Afrika, ambako si kama tu wamefahamu utamaduni wa nchi mbalimbali za Afrika, bali pia wamejionea historia na hali ya sasa ya urafiki na mawasiliano kati ya China na Afrika. 

 

Katika wiki mbili zijazo, wanafunzi hao watashiriki kwenye shughuli mbalimbali ikiwemo kujifunza lugha ya Kichina, kutembelea miji ya China na kujionea urithi wa utamaduni wa China, ili kuimarisha uelewa wao kuhusu lugha, utamaduni na jamii ya China.