Polisi ya Uganda ilisema kundi la waasi la ADF la Uganda tarehe 16 lilishambulia shule moja ya Uganda na kusababisha vifo vya watu 41.
Akigusia tukio hilo alipozungumza na wanahabari, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Mao Ning alisema China inalaani vikali shambulizi la mabavu dhidi ya raia hasa wanafunzi, na kutoa salamu za pole kwa majeruhi na rambirambi kwa familia za marehemu.
Mao alisisitiza kuwa China inapinga kitendo cha aina yoyote cha mabavu na kigaidi, na itaendelea kuunga mkono kithabiti jitihada za Uganda katika kulinda usalama wa nchi na utulivu wa jamii.