Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameagiza askari zaidi kupelekwa magharibi mwa nchi hiyo ambako watu wenye silaha wenye uhusiano na kundi la IS waliwaua wanafunzi 37 wa shule ya sekondari.
Wafuasi wa kundi la ADF walifanya mauaji hayo ijumaa jioni katika Shule ya Sekondari Lhubirira iliyoko Mpondwe, karibu na mpaka wa Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Jeshi na Polisi nchini humo pia wamesema washambuliaji hao wamewateka nyara wanafunzi sita na kukimbilia katika Hifadhi ya Taifa ya Virunga iliyoko mpakani mwa nchi hizo mbili, na mpaka sasa hatma ya wanafunzi hao haijulikani.