Waziri Mkuu wa China kuhudhuria Mkutano wa Baraza la Uchumi Duniani Davos
2023-06-21 10:10:06| CRI

Waziri Mkuu wa China Li Qiang anatarajiwa kuhudhuria Mkutano wa 14 wa Mwaka wa Baraza la Uchumi Duniani Davos, utakaofanyika Juni 27 huko Tianjin.

Akitoa taarifa hiyo jana Jumanne msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Mao Ning, alisema Waziri Mkuu Li atahudhuria sherehe ya ufunguzi, atatoa hotuba muhimu, na kukutana na Mwenyekiti Mtendaji wa Baraza la Uchumi Duniani Klaus Schwab na viongozi wengine mashuhuri wa kigeni, pamoja na viongozi wa biashara wa kimataifa wa Baraza la Uchumi Duniani.

Waziri Mkuu wa Barbados Mia Amor Mottley, Waziri Mkuu wa Mongolia Luvsannamsrai Oyun-Erdene, Waziri Mkuu wa New Zealand Chris Hipkins, Waziri Mkuu wa Vietnam Pham Minh Chinh na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani Ngozi Okonjo-Iweala watahudhuria mkutano huo wa kila mwaka.