Katibu Mkuu wa chama cha African National Congress (ANC) Fikile Mbalula amesema kuwa Afrika Kusini inatetea suluhu za amani kwenye mzozo unaoendelea kati ya Russia na Ukraine.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa pamoja na viongozi na wawakilishi kutoka nchi nyingine sita za Afrika wamekutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Rais wa Russia Vladimir Putin mwishoni mwa wiki iliyopita, na kuwasilisha mpango wenye vipengele 10 unaolenga kuleta mchakato wa amani.
Mbalula amesema ujumbe wa amani wa Afrika unaoongozwa na Ramaphosa haupaswi kudharauliwa, kwa sababu ni mpango muhimu katika juhudi za kuleta suluhu ya amani kwa mzozo kati ya Ukraine na Russia. Mpango huo unaotaka kusitishwa kwa mapigano na kufanya mazungumzo utaufanya mzozo huo kukaribia kwisha.