Waziri mkuu wa China asema China inapenda kufunguliana zaidi milango na Ufaransa
2023-06-22 09:37:13| CRI

Waziri mkuu wa China Bw. Li Qiang Jumatano aliwasili mji wa Paris na kufanya ziara rasmi nchini Ufaransa. Li alisema Ufaransa ni mjumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na nchi kubwa yenye moyo wa kujiamulia, pia ni mwenzi wa kimkakati wa pande zote wa China. Uhusiano kati ya China na Ufaransa unadumisha maendeleo ya kiwango cha juu, na unabeba umuhimu mkubwa duniani unaozidi kiwango cha pande mbili.

Li alisema, mwezi Aprili mwaka huu, rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron, walifikia makubaliano mfululizo ya kimkakati, kuweka mwongozo wa uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Ufaransa, na kutoa mwelekeo kwa ushirikiano kati ya China na Ufaransa kwenye kiwango cha pande mbili, China na Ulaya na dunia.

Aliongeza kuwa China inapenda kushirikiana na Ufaransa katika kufunguliana zaidi milango yao, kujenga mnyororo imara wa kiviwanda na usambazaji kati ya China na Ufaransa na kati ya China na Ulaya, kuzidisha mawasiliano na kufundishana kati ya watu, kushirikiana katika kukabiliana na changamoto za dunia kama vile mabadiliko ya tabianchi na maendeleo endelevu, ili kutia nguvu mpya kwenye ukuaji endelevu, mzuri na tulivu wa uhusiano kati ya China na Ufaransa, na kutia imani na nguvu zaidi kwa amani, utulivu na maendeleo ya dunia. China inapenda kushirikiana na Ufaransa katika kuufanya mwongozo wa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Ufaransa uliowekwa na viongozi wa nchi mbili uwe mipango kazi na kutimizwa.