Waziri mkuu wa China afanya ziara nchini Ufaransa na kuhudhuria mkutano wa kilele wa makubaliano ya uwekezaji duniani
2023-06-23 14:22:36| CRI

Waziri mkuu wa China Li Qiang amewasili Paris, mji mkuu wa Ufaransa, na kuanza ziara rasmi nchini humo, ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria na kuhutubia mkutano wa kilele wa makubaliano ya uwekezaji duniani.

Akizungumza na wanahabari katika uwanja wa ndege, Li amesema uhusiano wa China na Ufaransa umedumisha maendeleo ya kiwango cha juu, na una maana ya kimataifa inayozidi nchi hizo mbili. Ameongeza kuwa China inapenda kushirikiana na Ufaransa kukabiliana na changamoto za kimataifa kwa pamoja, na kuongeza nguvu zaidi kwa amani, utulivu na maendeleo duniani.

Katika ziara hiyo, Li atakutana na rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, kufanya mazungumzo na waziri mkuu wa nchi hiyo Elisabeth Borne