Waziri mkuu wa China Bw. Li Qiang amesema maendeleo ya China yanatoa fursa na wala sio hatari kwa dunia, na yanaleta utulivu na wala sio mitikisiko kwenye mnyororo wa viwanda na ugavi duniani.
Kwenye mkutano kati yake na mkuu wa Baraza la Ulaya Charles Michel kando ya Mkutano wa Kilele kuhusu Mkataba Mpya wa Kifedha Duniani, Bw. Li Qiang amesema China inatumai kuwa Umoja wa Ulaya utauangalia ushirikiano wake na China kwa mtazamo wa kimantiki unaozingatia ukweli, na kufanya kazi pamoja na China ili kulinda mazingira mazuri kwa ajili ya ushirikiano wa kiutendaji kati ya pande hizo mbili.
Bw. Li Qiang amesema, China inapenda kufanya juhudi za pamoja na Umoja wa Ulaya katika kuimarisha utulivu na uhakika wa uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya pande hizo mbili, ili ziweze kupata matokeo makubwa zaidi ya kunufaishana.