Umoja wa Afrika watoa mafunzo kwa askari polisi wa Somalia kuwasaidia kuboresha ujuzi wa kuongoza magari na usalama barabarani
2023-06-26 08:29:18| CRI

Tume ya Mpito ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (ARMIS) imesema imekamilisha mafunzo ya wiki mbili kwa askari 55 wa usalama barabarani wa nchini Somalia ili kuimarisha uwezo wao wa kusimamia usafiri wa magari na kuhakikisha usalama katika barabara za umma.

Tume hiyo imesema mafunzo hayo yaliyomalizika ijumaa iliyopita yalifanyika kwa pamoja katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, mji wa Jowhar mkoa wa Hirshabelle, Baidoa mkoa wa Kusini Magharibi, na Kismayo katika mkoa wa Jubaland.

Akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo hayo, Kamishna wa Jeshi la Polisi la ATMIS Hillary Sao Kanu amewataka askari polisi hao kubadilishana uzoefu waliopata ili kuimarisha utoaji wa huduma hiyo.

Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi nchini Somalia Osman Abdullahi Mohamed amesema, mafunzo hayo yatasaidia kubadili usimamizi wa magari katika miji ya nchi hiyo inayokabiliwa na msongamano mkubwa wa magari.