Magari 49 yawaka moto katika shindano la mbio za magari nchini Botswana
2023-06-26 08:28:42| CRI

Magari 49 yamewaka moto katika mji wa madini wa Jwaneng, kusini mwa Botswana jana mchana kwa saa za huko, ambako wamiliki wa magari hao walikuwa wanashiriki Shindano la Mbio za Magari Jangwani la Kampuni ya Toyota.

Waliporejea kutoka kutazama Mbio hizo, wamiliki wa magari hayo walikuta yakiwaka moto huku mengine yakiwa yameteketea kabisa.

Hakuna vifo vilivyoripotiwa mpaka sasa, na Polisi wanaendelea na uchunguzi kujua chanzo cha moto huo.