Uganda inapanga kuongeza umri wa kuanza kunywa pombe hadi miaka 21
2023-06-26 22:35:28| cri

Serikali ya Uganda imetangaza mpango wa kuongeza umri halali wa kuanza kunywa pombe kutoka miaka 18 ya sasa hadi 21. Ripoti ya takwimu za Afya Duniani 2023 zinaitaja Uganda kuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa viwango vya juu vya unywaji wa pombe. Ripoti ya WHO, inakadiria kuwa waganda kwa sasa hutumia lita 12.2 za pombe kwa kila mtu kwa mwaka, kiasi ambacho ni kikubwa zaidi kuliko wastani wa kimataifa.

Kamishna wa Wizara ya Afya anayeshughulikia afya ya akili, pombe na dawa za kulevya wa Uganda Dk. Hafsa Lukwata, amesema utafiti umeonyesha kuwa ikiwa mtu hajatumia kilevi kabla ya kufikia umri wa miaka 21, ana uwezekano mdogo wa kutumia vileo baadaye maishani.