Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China atoa maoni kuhusu tukio la kundi la Wagner
2023-06-26 16:34:24| cri

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China amesema China ikiwa ni jirani na rafiki wa Russia na mwenzi wake wa kimkakati kwa pande zote katika zama mpya, inaiunga mkono Russia  kudumisha utulivu wake na kutimiza maendeleo na ustawi.

Habari zimesema mwanzilishi wa Kundi la Wagner Yevgeny Prigozhin na vikosi vyote vya Wagner wameondoka kutoka makao makuu ya kamandi ya kusini ya jeshi la Russia.

Bw. Prigozhin amekubali pendekezo la Rais wa Belarus Alexander Lukashenko kwa kundi hilo kusitisha operesheni zake nchini Russia, na kuchukua hatua zaidi za kupunguza hali ya wasiwasi. Rais wa Russia Vladimir Putin ametoa hakikisho kwamba Bw. Prigozhin anaweza kwenda Belarus na Russia itafuta mashtaka ya jinai dhidi yake.

Msemaji huyo amesema kuwa tukio la kundi la Wagner ni jambo la ndani la Russia.