Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za rambirambi kwa mwenzake wa Uganda Yoweri Museveni kufuatia shambulizi dhidi ya shule moja lililotokea magharibi mwa nchi hiyo na kusababisha vifo na majeruhi ya watu wengi.
Rais Xi ametoa rambirambi kutokana na vifo vya watu wasio na hatia kwenye shambulizi hilo, na kutoa pole kwa familia za wafiwa na majeruhi.
Rais Xi ameeleza kuwa China inalaani vitendo vya kigaidi vya aina zote na itaendelea kuunga mkono kwa dhati juhudi za Uganda kupambana na ugaidi na kulinda usalama na utulivu wa taifa.