Naibu mjumbe wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing ameeleza wasiwasi wa China juu ya kuendelea kwa tishio la makundi yenye silaha kwa utulivu wa eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Akizungumza jana kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja huo kuhusu suala la DRC, Balozi Dai amesema, China inayataka makundi yenye silaha kuacha mara moja vitendo vyao vya ukatili, kujiondoa katika maeneo yanayodhibiti, na kuanza mchakato wa kuwapokonya silaha na kuyaondoa makundi ya wapiganaji katika maeneo hayo.
Amesema China inapongeza operesheni za pamoja za DRC, Uganda na Burundi ili kukabiliana na vitisho vya pamoja, na kwamba inatumai kuwa hatua husika za kikanda zitaimarisha uratibu ili kupunguza hali mbaya ya usalama katika kanda hiyo.