UNHCR yasema wakimbizi zaidi ya milioni 2.4 watahitaji kupata makazi mapya katika mwaka 2024
2023-06-27 08:37:05| cri

 

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) jana limesema, zaidi ya wakimbizi milioni 2.4 watahitaji kupata makazi mapya katika mwaka 2024, ikiwa ni ongezeko la asilimia 20 kuliko mwaka 2023.

Kutokana na ripoti ya tathmini kuhusu Makadirio ya Mahitaji ya Makazi Mapya Duniani, Asia iko nafasi ya kwanza katika orodha ya mahitaji ya mwaka 2024, na wakimbizi karibu elfu 730 watahitaji kupata makazi mapya, na kuchukua asilimia 30 katika mahitaji ya dunia nzima.

Kutokana na kuendelea kwa mgogoro wa Syria, wakimbizi 754,000 wanahitaji kupata msaada wa dharura kwa kupitia kupewa makazi mapya.