Rais wa China akutana na mawaziri wakuu wa Mongolia, Vietnam, Barbados na New Zealand
2023-06-27 22:10:27| CRI

Rais Xi Jinping wa China leo kwa nyakati tofauti amekutana na mawaziri wakuu wa Mongolia, Vietnam, Barbados na New Zealand ambao wako ziarani nchini China.

Katika mazungumzo na waziri mkuu wa Mongolia Luvsannamsrai Oyun-Erdene, rais Xi amesisitiza kuwa China na Mongolia zinatakiwa kushikilia kuheshimiana uhuru, mamlaka na ukamilifu wa ardhi wa nchi hizo mbili, kuheshimu njia ya maendeleo ambayo watu wa nchi hizo mbili walijiamulia, na kuungana mkono kithabiti maslahi kuu na masuala muhimu ya nchi hizo mbili.

Kwa upande wake Oyun-Erdene ameeleza kuwa Mongolia inapenda kushirikiana na China kuujenga uhusiano kati ya pande hizo mbili kuwa mfano mzuri wa kuigwa.

Wakati alipokutana na waziri mkuu wa Vietnam Pham Minh Chinh, rais Xi amesema kutokana na hali ya utatanishi duniani, China na Vietnam zinatakiwa kushirikiana na kutafuta maendeleo ya pamoja, ili kuleta utulivu kwa dunia.

Naye Pham Minh Chinh ameeleza kuwa chama na nchi ya Vietnam siku zote zinaunga mkono kithabiti Kamati Kuu ya CPC inayoongozwa na rais Xi Jinping na awamu mpya ya uongozi wa China.