Hafla ya kufunga Kambi ya Majira ya Joto kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari wanaosoma lugha ya Kichina nchini Tanzania yafanyika
2023-06-28 15:22:08| cri

Hafla ya kufunga Kambi ya Majira ya Joto kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari wanaosoma lugha ya Kichina katika Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanzania imefanyika Juni 27, 2023 katika Chuo Kikuu cha ualimu cha Zhejiang, ikiashiria kumalizika kwa mafanikio kwa ziara ya wanafunzi kutoka Tanzania nchini China. Kambi hii ya majira ya joto ni ya kundi la kwanza kufanyika katika Chuo Kikuu hicho baada ya janga la COVID-19, na sehemu zilizotembelewa ni pamoja na Beijing, Jinhua, na Shanghai. Katika wiki hizo mbili za Kambi hiyo, wanafunzi hao waliongeza uelewa wao wa lugha ya Kichina, utamaduni na jamii kupitia shughuli mbalimbali ikiwemo urithi wa utamaduni usioshikika. Tuwatazame baadhi ya wanafunzi na mwalimu wao wakizungumzia waliyojifunza katika ziara hiyo.