Watu 11 wauawa katika shambulizi la risasi nchini Honduras
2023-06-28 08:31:01| CRI

Polisi nchini Honduras imethibitisha kuwa, watu 11, akiwemo mwanamke mmoja, wameuawa na wengine watatu kujeruhiwa katika tukio la shambulio la risasi lililotokea jumamosi usiku kwenye ukumbi wa mchezo wa biliadi kaskazini mwa Honduras.

Shambulio hilo limetokea katika mji wa Choloma, wilaya ya Cortes, ambapo watu waliokuwa na silaha nzito walipovamia ukumbi huo na kufyatua risasi.

Rais wa Honduras Iris Xiomara Castro Sarmiento ametangaza marufuku ya kutembea usiku katika eneo hilo kutokana shambulio hilo.