Taarifa kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini China inasema kuwa rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt Hussein Mwinyi anafanya ziara ya kikazi nchini China kuanzia Juni 27, 2023.
Katika ziara hiyo Rais Mwinyi atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi waandamizi wa serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na pia anatarajiwa kushiriki katika maonesho ya 3 ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika akiwa kama mgeni rasmi. Maonesho hayo yatafunguliwa kesho tarehe 29 Juni.
Aidha rais Mwinyi anatarajiwa kushiriki katika hafla ya utiaji saini mkataba wa ushirikiano baina ya hospitali ya watoto ya Hunan na hospitali ya Taifa ya Muhimbili pamoja na Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar, ambapo kupitia ushirikiano huo wataalamu wa Tanzania watapatiwa mafunzo ya kujenga uwezo pamoja na hospitali hizo kupata msaada wa upanuzi wa wodi za watoto.
Rais mwinyi pia anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa makampuni yenye nia ya kuwekeza katika sekta mabalimba nchini Tanzania.