Waziri mkuu wa China ahutubia ufunguzi wa Baraza la Davos
2023-06-28 08:33:20| cri


 

Waziri mkuu wa China Bw. Li Qiang jana asubuhi ameshiriki kwenye ufunguzi wa Baraza la Davos la Majira ya Joto lililofanyika huko Tianjin, China, ambalo limehudhuriwa na mwenyekiti wa Baraza la Uchumi Duniani (WEF) Klaus Schwab, Mkurugenzi wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) Ngozi Okonjo-Iweala, mawaziri mkuu wa Barbados, Mongolia, New Zealand na Vietnam, na wajumbe 1500 kutoka nchi na sehemu zaidi ya 90.

Akihutubia ufunguzi wa Baraza hilo, Li Qiang amesema China inapenda kushirikiana na kampuni za nchi mbalimbali, kuunga mkono kithabiti utandawazi wa dunia wa kiuchumi, kulinda uchumi wa soko, kuunga mkono biashara huria, na kuongoza uchumi wa dunia kuelekea mustakabali wa kunufaisha pande nyingi zaidi.