Wanasayansi wa China na Afrika watoa wito wa kuwa mfumo nyumbufu wa vyakula vinavyohimili ukame ili kukabiliana na njaa
2023-06-28 08:32:45| CRI

Wanasayansi wa China na Afrika wamerejea wito wao wa kuongeza mifumo ya kilimo ambayo inaendana na asili na nyumbufu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi ili kukabiliana na njaa na utapiamlo.

Wakizungumza katika jukwaa lililofanyika jana jumatatu mjini Nairobi, Kenya, wanasayansi hao wamezungumzia kuongezeka kwa mgogoro wa njaa barani Afrika, huku wakisisitiza kuwa suluhisho la kudumu linategemea kuhamia kwenye kilimo cha vyakula vinavyostahamili mabadiliko ya tabianchi.

Wanasayansi 100 kutoka China na Afrika wanahudhuria jukwaa hilo linalohusu hali ya hewa, mfuko wa ikolojia, na maisha ili kujadili njia za uvumbuzi zitakazoboresha usalama wa chakula na lishe barani Afrika.