Kilo 315 za dagaa wa maji chumvi kutoka Kenya zimewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Huanghua, Changsha, China, jumatatu wiki hii, ikiwa ni mara ya kwanza kwa China kuagiza bidhaa hiyo kutoka Kenya.
Katika miaka ya karibuni, China imeongeza kasi ya uagizaji wa mazao ya kilimo kutoka barani Afrika, na kuwa nchi kubwa ya pili inayoagiza mazao ya kilimo kutoka Afrika.
Katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka huu, China iliagiza mazao ya kilimo na chakula yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 2.23 kutoka Afrika, na kuongezeka kwa asilimia 26.5 kuliko mwaka jana wakati kama huo.