Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Xi Jinping ametoa wito wa kujifunza vyema fikra muhimu za Kamati Kuu ya CPC kuhusu ujenzi wa Chama, na kuboresha kazi za Chama.
Xi, pia ni rais wa China na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi, alisema hayo katika maagizo ya hivi karibuni. Maagizo hayo yalisomwa katika mkutano wa kitaifa wa kazi za Chama, ambao ulifanyika Jumatano na Alhamisi.
Xi, kwa niaba ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, alitoa salamu kwa wanachama wote wa Chama wakati Chama hicho kitaadhimisha miaka 102 tangu kuanzishwa kwake Julai 1.