Mwanariadha wa mbio ndefu wa Tanzania, Gabriel Geay, ameibuka na ushindi katika mbio za kilomita 10 za Boston zilizofanyika Boston, Marekani, Jumapili.
Geay alitumia muda wa dakika 27.49 na kuondoka na medali ya dhahabu katika mbio ambazo wanariadha kutoka majimbo 49 na nchi 102 walishiriki mbio za maili 6.2 kupitia Back Bay. Geay alitia kibindoni dola 10,000 (Sh24 milioni).
Huu ni ushindi wake wa pili katika mbio za 10K za Boston ndani ya miaka mitano. Mwanariadha huyo alishinda medali ya kwanza ya dhahabu katika mbio hizo mwaka 2018 baada ya kutumia dakika 28:24, huku Mkenya Mary Wacera akishinda mbio za wanawake kwa dakika 31:55. Mbio hizo zimemshuhudia Mkenya Edwin Kurgat akishika nafasi ya pili baada ya kutumia dakika 28:01 na mwenzake Alex Masai aliyeshika nafasi ya tatu kwa dakika 28.09.