Pande mbili zinazopambana nchini Sudan zatangaza kusimamisha vita kwa muda
2023-06-29 08:35:37| CRI

Pande mbili zinazopambana nchini Sudan hivi karibuni zimetangaza kusimamisha vita kwa muda kabla ya Sikukuu ya Eid al-Adha.

Jumanne wiki hii, Kamanda mkuu wa jeshi la Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan alitangaza kuwa jeshi hilo litasimamisha vita jana Jumatano, huku kiongozi wa Kikosi cha RSF, Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo akitangaza kuwa kikosi hicho kitasimamisha vita kwa siku mbili kuanzia Jumanne, na kuwaachia huru mateka 100 wa jeshi la Sudan.

Vyombo vya habari vya nchi hiyo vimeripoti kuwa, pande hizo mbili ziliendelea kupambana katika maeneo mengi huko Khartoum, mji mkuu wa nchi hiyo, siku ya Jumanne.