Wanawake wanakabiliwa na changamoto nyingi, hususan za kiafya. Afya bora ndio msingi wa maendeleo kwa kila jamii, na kama suala la afya halitatiliwa mkazo, ina maana kuwa jamii husika itakuwa na wakati mgumu wa kupata maendeleo kwani mtu ni afya. Wanawake na wasichana wengi duniani wanakabiliwa na maumivu makali wanapokuwa kwenye hedhi, yanayotambuliwa kitaaluma kama Endrometriosis, na wengi wao wanakosa tiba kutokana na imani kuwa, maumivu wakati wa hedhi ni jambo la kawaida. Kipindi chetu cha Ukumbi wa Wanawake hii leo kitazungumzia zaidi ugonjwa huu wa Endometriosis, na jinsi gani msichana ama mwanamke anaweza kujua ana ugonjwa huo, pamoja na tiba yake.