Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia Meles Alem amesema Ethiopia inatarajia kupata majibu mazuri juu ya ombi lake la kujiunga na nchi wanachama wa BRICS.
Akiongea kwenye mkutano na vyombo vya habari, kama ilivyonukuliwa na shirika la habari la ENA, Mwanadiplomasia huyo alisema wanatarajia BRICS itawapa jibu muafaka kwa ombi ambalo wametoa na kusisitiza kuwa Ethiopia imetuma maombi rasmi ya kujiunga na muungano huo.