Tume ya Mpito ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) jana imesema, imekamilisha kipindi cha kwanza cha kuondoa askari wake nchini Somalia, na kukabidhi vituo vya msingi vya kijeshi katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu na eneo la kusini.
Tume hiyo imesema, kambi ya mafunzo ya kijeshi cha Aljazeera One mjini Mogadishu na kambi ya Geriley iliyoko mkoa wa Jubaland vimekabidhiwa kwa vikosi vya usalama vya Somalia hapo jana.